Janga la DUNIA...Congo Yapata Mgonjwa Mwingine wa Corona | ZamotoHabari.

 
Waziri wa Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eteni Longondo, ametoa wito kwa raia wake kuzingatia usafi wakati wowote hii ni baada ya kuthibitisha kisa cha pili cha mtu mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona nchini humo.


Inadaiwa kuwa mtu huyo ni raia wa Cameroon aliyewasili nchini humo kutoka nchini Ufaransa, ambaye aliingia nchini humo, juma lililopita na alikuwa amewekwa karantini, baada ya uchunguzi aliofanyiwa katika uwanja wa ndege wa Kinshasa na kubaini kuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Kwa sasa anapatiwa matibabu katika kituo cha zamani cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola, Mashariki mwa Mji Mkuu wa Kinshasa.

Ikumbukwe kuwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya Corona nchini humo, kilithibitishwa siku ya Jumanne na Msemaji wa Wizara ya Afya, ambapo Congo ni nchi ya 11 barani Afrika, kuthibitisha maambukizi ya ugonjwa hatari wa COVID-19.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini