JE.WAJUA FAIDA ZA MICHE YA MCHIKICHI. | ZamotoHabari.


KIGOMA MA MAFUTA YA MAWESE;

Mafuta ya mawese ama palm oil yana faida nyingi tu kwa ajili ya ngozi yako Yanalainisha ngozi na kuiacha ikiwa na unyevu unyevu

Siku hizi sabuni, shampoo na mafuta mengi yanayotengenezwa viwandani yanakua yanatumiwa mafuta ya mawese kama malighafi ya kutengenezea. Hii ni kwa sababu ya ubora wake na suluhisho katika maswala yanayohusu ngozi.

Yana virutubisho vinavyoweza kuponesha ngozi iliyochomwa na jua na yenye michirizi Kama ilivyo kwa mafuta mengine halisi mafuta ya mawese ni bora sana kwa kuwa na virutubisho ambavyo ni asilia yani natural Vitamin E

Haya mafuta yana vitamin E inayojulikana kama tocotrienols. Tocotrienols imefanyiwa utafiti na ikagundulika kuwa ina nafasi katika kuishinda saratani(cancer) na magonjwa ya ubongo na moyo.

Pia inasaidia kujikinga na jua kali na kupunguza makovu. Hii ni kutokana na faida za tocotrienols iliyotajwa hapo juu.Vitamin K: Hii inasaidia ngozi iweze kuwa na uwezo zaidi wa kujiponya yenyewe mfano katika vidonda vidogo dogo na kupona haraka baada ya kufanyiwa upasuaji.

Glycolipids: Hii inasaidia kuifanya ngozi kuwa vizuri kuepuka ngozi kukakamaa au kuwa na ngozi ya uzee.
Wakulima wa miche ya michikichi katika eneo la mashamba ya Mugumile mkoani Kigoma wakichambua mbegu za miche hiyo kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya mawese. Mafuta ya mawese yanavitamini E Pia ya nafaida nyingi tu kwa ajili ya ngozi ya binadamu.(Pix Albart Jackson)
 
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini