Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus | ZamotoHabari.

Zaidi ya nchi 110 hadi sasa zimeripoti visa vya coronavirus na Shirika la Afya Duniani limetangaza virusi hivyo kuwa janga.

Yafuatayo ni majibu ya baadhi ya maswali ambayo wasomaji wamekua wakiyauliza.

1. Je inachukua kipindi gani mpaka mtu afahamike kuwa na coronavirus? - Swali lililoulizwa na Gillian Gibs

Inachukua siku tano kwa wastani kuanza kuonesha dalili, tangu mtu apate maambukizi, wanasayansi wamesema, lakini baadhi ya watu huanza kuonesha dalili hata baadae kuliko kipindi hiki.
Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona

Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema. Lakini baadhi ya watafiti wanasema kipindi hicho kinaweza kuchukua hadi siku 24.

Kufahamu na kuelewa kipindi cha ukuaji ni muhimu sana. Huwasaidia madaktari na mamlaka za afya kuanzisha njia bora za kudhibiti usambaaji wa virusi.

2. Je ukipona coronavirus ina maanisha unakinga ? RubyRed aliuliza kwenye ukurasa wa Twitter.

Kusema ukweli ni vigumu kuelezea. Virusi hivi vimekuwepo tu tangu mwezi Disemba, lakini kutokana na uzoefu wa virusi vingine na coronaviruses unatakiwa kuwa na kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na virusi ambayo itakulinda.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini