Meneja Afunguka Video Chafu Ya Abdu Kiba! | ZamotoHabari.


Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Abdul Kiba ‘Abdu’ kuposti video yake chafu ya ngono kwenye Mtandao wa Snapchat, meneja wake, Rehema Fussi amefunguka juu ya ishu hiyo.

Video hiyo ilisambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Abdu na mrembo ambaye hakutambulika mara moja wakishiriki vitendo vya ngono.

Kufuatia taarifa za kuwepo kwa video hiyo, baadhi ya watu walikuwa wakihaha kuomba ‘koneksheni’ watumiwe na kila mtu kusema lake.

Baadhi ya watu walionekana kukerwa na jambo hilo na kusema kwamba yeye (Abdu) kama kioo cha jamii hapaswi kuposti mambo yasiyo na maadili mitandaoni.

Wakati mambo yakiendelea kutaradadi mitandaoni, mwandishi wetu alimtafuta Abdu ambapo simu yake iliita bila kupokelewa.

Baadaye taarifa zilisambaa mitandaoni kuwa Abdu alisema aliibiwa simu, hivyo aliyeiba ndiye aliyesambaza video hizo chafu.

“Nilipoteza simu na kwa kuwa nina familia, huwa siweki password kwenye simu yangu.

“Huyo aliyeiba ndiye amepata urahisi wa kuposti video hiyo ili aniharibie,” ulisomeka ujumbe huo uliodaiwa kutoka kwa Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa King Kiba.

Baadhi ya watu walionekana kutokukubaliana na utetezi wake na kusema hiyo ndiyo tabia yake ya kurekodi wanawake akiwa nao faragha kisha kuwaomba pesa na wasipompa, huwatishia kuposti video zao mitandaoni.

“Nasikia anawaambia kaibiwa simu, ni muongo, huyu dada aliyenitumia screenshoot, besti yake alimpigia Abdu asubuhi na kumshtua kuwa umeharibu, he was like OMG, akapanic hatari na kufuta fasta.


“Anachokifanya Abdu huwa ni kutembea na majimama ya Kariakoo yenye maduka, then (kisha) anayarekodi, halafu anaanza kuya-black mail, wasipompa pesa anawatishia ataziachia video zao mitandaoni.

“Inabidi tu wamama wamlipe ili wasiharibu ndoa zao.

“In short ilikuwa 40 yake, alijua anarekodi kumbe yupo Snapchat, siku za mwizi ni 40,” aliandika mmoja wa watu kwenye moja ya kurasa za udaku za Instagram.

Baada ya kumkosa Abdu mwenyewe, mwandishi wetu alimtafuta meneja wake aliyetajwa kwa jina moja la Rehema na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo mambo yalikuwa hivi;

IJUMAA WIKIENDA: Kuna video chafu zinasambaa mitandaoni na watu wanasema ni msanii wako Abdu Kiba, maana aliiposti yeye mwenyewe kwenye akaunti yake ya Snapchat, una lipi la kuzungumza?


MENEJA: Kiukweli sijaiona hiyo video, ila nasikia tu watu wanasema huko mtandaoni. Sasa siwezi kuzungumza chochote kwa sababu tangu itokee hiyo ishu, hata Abdu mwenyewe sijaongea naye.

IJUMAA WIKIENDA: Lakini msanii wako ndiye anashukiwa kuhusika kwenye video hiyo, jina lake linaongelewa sana, huoni kama hii ishu inaweza kumshusha kimuziki?

MENEJA: Ni kweli unayosema, hiyo video inayoongelewa siyo nzuri ni mbaya na kiukweli mimi kama meneja najisikia vibaya sana msanii wangu kuhusishwa na kashfa kama hizo, lakini kama nilivyosema awali, siwezi kuzungumza lolote mpaka niione hiyo video na niongee na msanii wangu.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini