MVUA ZAZIDI KUHARIBU MIUNDO MBINU YA BARABARA | ZamotoHabari.


Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali hapa Nchini, zimendelea kuleta athari tofauti ikiwa ni pamoja uharibifu wa Miundo Mbinu ya Barabara na kusababisha adha Kwa wasafiri na wasafirishaji wa mizigo.

Ikiwa ni siku chache tangu kukatika daraja linalounganisha Barbara kuu ya Dodoma Morogoro, hali kama hiyo imejitokeza tena katika Barabara Kuu ya Lusahunga Biharamulo eneo la Nyambale, daraja dogo limepasuka kutokana na kulemewa wingi wa Maji yanayotiririka kutokea Vilima vya Jirani, na hivyo kupelekea kusitishwa Kwa Barabara hiyo kwa muda mpaka pale ufumbuzi ulipopatikana kwa kurekebisha njia mbadala na kisha kuruhusu Magari kuanza kupita eneo hilo

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera chini ya Mwenyekiti wake Brig. Jen Marco E. Gaguti imefika eneo hilo na kujionea kinachoendelea licha ya hatua za awali kuchukuliwa mapema kwa kuelekeza Magari yanayotumia njia hiyo, kuzunguka kupitia njia ya Runzewe na kutokea njia panda ya Mwanza, hatua ambayo imeondoa kero kwa wasafiri wa mabasi na kuendelea na safari zao kama kawaida.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio tayari Magari yaliyokuwa yamekwama yameruhusiwa kupita na kuendelea na safari, huku jitihada za makusudi zikiendelea kufanyika katika daraja lililopasuka ikiwa ni kulifumua upya na kuongeza upana wa kutatua tatizo la kudumu.






APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini