Mzee Yusuf Nini Kimemsibu TENA...Atangaza Kurudi Kwenye Muziki ‘Nitaimba Mpaka Nigaragare’ | ZamotoHabari.


ALIYEKUWA mwimbaji maarufu wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuf, amesema anatafuta pesa kwa ajili ya kurudi kwenye muziki ambapo alitangaza kuacha kufanya kazi hiyo miaka minne iliyopita na kuanza kumtumikia Mungu.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuongeza kuwa anafanya hivyo kutokana na pengo kubwa analoliona kwenye muziki kwa sasa.

“Wakati naanza muziki huu wa kidunia, nilikuwa nina mori kuliko Mmasai, ila muda ulipokwenda mori ikapungua kisha nikaacha kwa kuwa nilihisi sioni sababu ya kuendelea, cha kushangaza sasa hivi nina hamu ya kuimba balaa, nataka niimbe mpaka nigaragare mwaka huu,” ameandika.
“Nitaimba sana nikija mjini ila sijajua ni muziki gani kama ni kisingeli, kiduku au taarab, nimeacha kuimba miaka minne pengo lipo na ndiyo wakati wa kuzibwa sasa, kuimba hatujakatazwa kwa sasa natafuta nauli ya kurudi mjini,” amesema .



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini