NAIBU SPIKA WA BUNGE DK.TULIA AUPONGEZA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA KWA JITIHADA ZAKE ZA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KULETA MAENDELEO | ZamotoHabari.

 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier(wa nne kutoka kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya chakula cha usiku ambacho amekiandaa kwa ajili ya mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo nchini ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa.(wa watano kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson akiwa aliyeshiriki kwenya hafla hiyo.
 Naibu Spika Dk.Tulia Ackson akitoa pongezi kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier kutokana na jitihada zao za kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo. 
 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson ili kuzungumza na mabalozi mbalimbali walioko nchini ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na balozi huyo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwa ajili ya mabalozi ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa pamoja na wageni wengine waalikwa..
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa mabalozi walioko nchini Tanzania ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa ambaye pia ni  Balozi wa Morocco  nchini Abdelilah Benrayane akifafanua jambo wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Balozi Fr'eder'ic Clavier.
 Baadhi ya mabalozi wa nchi mbalimbali waliko nchini Tanzania wakiwa nyumbani kwa Balozi wa Ufaransa nchini Fr'eder'ic Clavier baada ya kuwaalika kwenye chakula cha usiku.Mabalozi hao wapo kwenye umoja wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa. 
 Balozi wa Ufaransa nchini Tazanzania Fr'eder'ic Clavier(kulia) akiteta jambo na Balozi wa Morocco  nchini Abdelilah Benrayane . 
 Naibu Spika Dk.Tulia Ackson akizungumza wakati wa hafla hiyo.Wengine ni mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa wakiwa na mwenyeji wao Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier(wa nne kutoka kulia).
 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 


 


 

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

NAIBU Spika Dk.Tulia Ackson ametoa pongezi kwa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania ikiwemo kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi na ushirikiano.

Dk.Tulia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'eder'ic Clavier kwa kuwashirikisha mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini ambao nchi zao zinazungumza lugha ya Kifaransa. 

Akizungumza zaidi  Dk.Tulia amesema kuwa uwepo wa ubalozi huo nchini kuna mambo mengi yamekuwa yakifanya na yenye tija kwa pande zote mbili na kuna haja ya kuendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimandeleo.

Kuhusu watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa, Dk.Tulia amesema kwanza anampongeza Balozi wa Ufaransa nchini kwa hatua ambazo wanazichukua katika kuhakikisha lugha hiyo inapata nafasi ya kuzungumzwa na watu wengi."Nimesikia balozi amesema kwamba wameongeza bajeti yao ya fedha kwa ajili ya kutoa fursa ya wananchi kujifunza kifaransa.Ni jambo nzuri sana kwa wananchi wakiijua lugha hiyo na nyingine nyingi."

Amefafanua yeye alijifunza Kifaransa akiwa kidato cha kwanza lakini Ubalozi wa Ufaransa nchini  Tanzania kupitia balozi wao wamekwenda mbali zaidi kwa kutaka sasa watoto waanze kujifunza lugha hiyo kuanzia shule za msingi na kuendelea.

Kuhusu ombi la Balozi Clavier la kutaka Tanzania kujiunga kwenye umoja wa nchi zinazozungumza Kifaransa, Dk.Tulia amejibu hawezi kuijibia Serikali lakini kama mwananchi wa kawaida anachokiona ni kwamba balozi huyo ameonesha nia njema huku akisisitiza nchi hizo pamoja na nyingine zimekuwa na mahusiano mazuri yakiwemo ya uchumi.

"Kwa mfano Watanzania ni sehemu ya Afrika Mashariki, ni sehemu ya upande wa SADC, ni sehemu ya AU kwa maana ya Afrika, hivyo ni jambo nzuri kama tutashirikiana nao kwa karibu kwenye nyanja nyingi na uchumi ni eneo moja wapo.Lakini hii ya lugha ni mojawapo katika mambo ya utamaduni, na ni jambo jema sana,"amesema Dk.Tulia.

Awali akizungumza wakati wa kuwakaribisha mabalozi , wageni waalikwa na wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla hiyo, Balozi Clavier alitumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo lugha ya Kifaransa inavyozungumzwa na wananchi wa mataifa mbalimbali duniani huku akisisitiza dhamira ya kuona Watanzania nao wanahamasika kwa kujifunza na kuilewa na ndio maana wametenga fedha maalum kwa ajili hiyo.

"Lugha ya Kifaransa ni moja ya lugha kubwa duniani, inazungumzwa katika nchi mbalimbali na leo hii uwepo wa sehemu ya mabalozi ambao nchi zao zinazungumza lugha hii ni ushahidi mwingine wa kiasia gani inakubalika na kuwa sehemu ya mawasiliano kwa wananchi.Ndio maana tuna mabalozi wa kila nchi kwenye hafla hii ambayo nao wanazungumza Kifaransa.

"Hivyo tumeamua kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha nchi ya Tanzania watu wake wanajifunza lugha hii na tutatafurahi iwapo siku moja nao watakuwa sehemu ya zile nchi ambazo zinazungumza Kifaransa,"amesema Balozi Clavier.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa mabalozi walioko nchini Tanzania ambao nchi zao zinazungumza lugha hiyo ambaye pia ni Balozi wa Morocco  Abdelilah Benrayane amesisitiza kuwa kuna umuhimu kwa wananchi kuendelea kujifunza lugha hiyo pendwa duniani.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini