Rais wa Kenya afuta safari ya Italia kutokana na hofu ya corona | ZamotoHabari.




Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefuta safari yake ya Italia kufuatia hofu ya ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona. Baada ya China, Italia sasa ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa na kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, hadi kufikia Machi 14, watu 17,660 walikuwa wameambukizwa kirusi cha corona Italia huku wengine 1,268 wakiwa wamepoteza maisha.

Kwa mujibu wa ripoti katika gazeti la Daily Nation, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imeufahamisha Ubalozi wa Italia mjini Nairobi kuwa Rais Kenyatta amefuta safari yake ya Italia iliyotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 10 hadi 14.
 
 Rais Kenyatta alikuwa amepangiwa kutembelea mji mkuu wa Italia, Roma kwa lengo la kukutana na viongozi wa nchi hiyo na kisha aelekee Vatican kwa ajili ya kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis.
 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini