Mimba kuharibika au kutoka ni hali ya mimba yenye wiki 28 au chini ya hapo kuharibika au kutoka. Hali hujulikana kama miscarriage au spontaneous abortion kwa kiingereza. Mtoto aliye tumboni katika umri huu hataweza kuishi nje ya tumbo la mama. Katika nchi zilizoendelea huchukuliwa mimba iliyo chini ya kipindi cha wiki 24.
Zaidi ya asilimia 80 ya mimba huharibika katika miezi 3 ya kwanza ya ujauzito. Baada ya miezi hii kupita, uwezekano wa mimba kuharibika hupungua.
Dalili Za Mimba Kuharibika
Karibu asilimia 50 ya mimba zote huharibika hata kabla ya mwanamke kujua kama ni mjamzito, hasa ikisababishwa na matatizo katika vinasaba vya mtoto (congenital chromosomal abnormalities). Kwa mimba zilizoanza kukua dalili za mimba kutoka huwa ni
Kutokwa Damu Kwenye Uke. Damu inaweza kutoka kama matone kwenye nguo za ndani na baadae damu nyingi, au damu nyingi kama ya hedhi.Maumivu ya Tumbo. Mara nyingi hutokea chini ya kitovu. Yanaweza kuwa makali sana.Kutoa tishu, mabonge ya damu na mabaki ya kiini tete.Homa. Unaweza kupata homa kama mji wa uzazi ukipata maambukizi wakti mimba inaharibika.
Sababu Za Mimba Kuharibika
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mimba kuharibika zikiwemo;
Matatizo ya maumbile ya mtoto tumboni (genetic abnormalities)Maambukizi ya magonjwa wakati ujauzitoVivimbe vya tumbo la uzazi (uterine fibroids)Kovu kwenye tumbo la uzazi kutokana na kusafisha mimbaShingo ya uzazi kulegeaUgonjwa wa kisukariUgonjwa wa tezi ya shingo (hyperthyroidism)Uchunguzi na Vipimo
Pale unapopata dalili hizi, wahi kituo cha afya haraka. Hii itasaidia kuokoa maisha yamtoto ikiwezekana na yako!
Mtaalamu wa afya atakufanyia uchunguzi wa tumbo na via vya uzazi ikijumuisha kutazama tumbo, uke na shingo ya uzazi kama imefunga au la.
Vipimo ambavyo vinaweza kufanyika ni;
Kipimo cha mkojo cha ujauzito (Urinary Pregnancy Test)Ultrasound ya Tumbo. Huonesha sehemu mimba ilipopandikizwa, hali ya mtoto tumboni na maumbile yake.Vipimo vya damu kupima wingi wa damu huweza kufanyika pia.
Matibabu
Baada ya uchunguzi na vipimo, matibabu hutolewa kutokana na hali ya mimba ilivyo. Mimba inaweza kuwa;
Imeharibika na kutoka (complete abortion)Imeharibika lakini bado ipo kwenye mji wa uzazi (incomplete abortion)Kama mimba imeharibika na kutoka, basi utapewa dawa za kutumia ili kuzuia maambukizi ya vijidudu vya bakteria (antibiotics) na za kuongeza damu hasa kama ulitokwa na damu nyingi.
Kama mimba imeharibika lakini bado haijatoka yote, basi mji wa uzazi utahitaji kusafiswa. Kuna njia mbili ambazo hutumika kusafisha mji wa uzazi nazo ni;
Kuusafisha kwa kuvuta (Manual Vacuum Aspiration)
Njia hii hutumika pale ambapo mimba ina chini ya wiki 12. Kifaa maalumu huingizwa kwenye mji wa mimba na kuvuta uchafu mpaka utakapoisha. Huleta maumivu makali, hivyo unaweza ukapewa dawa ya ganzi au kuzuia maumivu.
Kusafisha mfuko wa uzazi kwa kuuwangua (Dilatation and Curretage)
Njia hii hutumika kama mimba ni kubwa zaidi ya wiki 12. Shingo ya uzazi hutanuliwa na kisha curreter huingizwa ambayo hukwangua mji wa uzazi kuondoa masalia ya mimba au mimba iliyobaki. Njia hii husababisha maumivu makali, utapewa dawa ya usingizi, ganzi au kuondoa maumivu wakati zoezi hili linafanyika.
Baada kusafiswa utapewa dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria na dawa za kuongeza damu ikibidi.
Baada Ya Mimba Kutoka
Baada ya mimba kutoka hakikisha unatumia dawa za kuua bakteria (antibiotics) kwa siku 5 mpaka 7.
Zingatia yafuatayo:
Unaweza ukaendelea kupata maumivu kwa siku kadhaa, lakini yatakuwa yanapungua polepole.Damu inaweza ikaendelea kutoka kidogo kwa muda wa wiki mojaUnaweza kuanza kufanya mapenzi baada ya damu kuacha kabisa, kama wiki 2 toka mimba kutoka.
Rudi haraka hospitali ikiwa;
Maumivu ya tumbo kuongezeka kadri siku zinavyoendaDamu nyingi inatoka ukeniUnapata homa
Kupata Ujauzito Tena
Kumbuka unaweza kupata ujauzito wiki 2 baada ya mimba kutoka. Tunashauri kusubiri kwa muda usiopungua miezi 3 kabla ya kupata mimba tena, ili kuruhusu viungo vipone vizuri na kuwa tayari kutunga mimba nyingine.
Wakati huu chagua njia salama ya kuzuia mimba utakayotumia na mwenzi wako. Shauriana na mtaalamu wa afya ili ujue aina ya njia unazoweza kutumia.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments