TAKUKURU KAGERA WALIVYOFANIKISHA KUREJESHA FEDHA ZA WASTAAFU KUTOKA TAASISI YA MIKOPO . | ZamotoHabari.

Na Abdullatif Yunus -  Michuzi TV.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa hapa Nchini TAKUKURU Mkoa wa Kagera inaendelea kuchunguza na kubaini Taasisi za kifedha ambazo zinajihusisha na Utoaji wa Mikopo kwa Riba kubwa tofauti na mikataba husika, huku Wananchi wakisahuriwa kukopa Fedha Benki ambazo riba zao ni nafuu.

Ushauri huo uliotolewa na Kaimu Mkuu wa Takukuru,Mkoa wa Kagera,Ndg Hassan W.Mossi ammbae amewataka wananchi na wastaafu kuwa makini pindi wanapokopa kwa kampuni za ukopeshaji,  ni vyema kukopa katika Benki kwani riba zao ni nafuu na  mikataba yao ipo wazi, na kuongeza kuwa wanapokopa wachukue kopi ya mikataba, wasiache kwa wakopeshaji kadi zao za Benki ni makosa pia kutokutoa Nywilwa(password )za akaunti zao.

Hali hiyo imetokana na  tukio la hivi karibuni la kukabidhiwa kwa Wastaafu watano kiasi cha fedha Shilingi Milioni kumi kufuatia uchunguzi huo kukamilika,  ukihusisha  Vyombo vya Usalama,   na kubaini Taasisi ya Mikopo ya ANNY CREDIT Co. LTD ya Wilayani Karagawe, ambayo imekuwa ikituhumiwa kwa kuchukua riba kwa kubwa kwa wakopeshaji wake wakiwemo wastaafu tofauti na riba waliyokubaliana.                     

Wastaafu hao wamedaiwa kufika kwa Bwn. Marwa  Machera Marwa ambae ni Mkurugenzi wa ANNY CREDIT Co. Ltd kuchukua fedha kwa lengo la kukopa ikiwa makubaliano ni kurejesha asilimia mkopo huo ndani ya muda waliokubaliana ikiwa ni pamoja na riba 17% lakini jambo ambalo limekuwa tofauti na badala yake wamekuwa wakikatwa fedha nyingi katika mfuko wao wa mafao ya pensheni.

Kilio hicho kinamfikia Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwataka TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo mara baada ya kubaini ukweli ndipo TAKUKURU wakafanikisha kurejesha kiasi cha fedha kutoka Taasisi hiyo ya Mikopo.

Miongoni mwa Waliokabidhiwa pesa hiyo ni pamoja na Mwalimu Mstaafu Chrispin Christinian aliyestaafu Mwaka 2018 amabaye amekaririrwa akisema "Tunamushukuru Mkuu wa Mkoa ,Mara nyingi unapostaafu mafao yanapokuwa yanaandaliwa inabidi ujikope,lakini tulishangazwa na gharama pale mafao yalipokuja ,tulijikuta tunakatwa fedha nyingi mnoo,tukaona ni vyema tushitaki kwa Mkuu wa Mkoa,tunaiomba Serikali ichunguze hizi tasisi maana mikataba na riba ni vitu viwili tofauti " Alisema christian.

Wengine waliopokea kiasi cha fedha shilingi Milioni Mbili kila mmoja na Mwaka wao wa kustaafu kwenye mabano ni  Bi. Florida Damian Kabeijuma (2017), Mwl. Benetson Sospeter Ngambeki (2018), Mwl. Revelian Kikangi Rukonge (2018), na Mwl. Augstine N. Yohana (2018).

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco Gaguti akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watumishi na wananchi kwa ujumla kama alivyokaririwa akisema "Natoa wito kwa watumishi kujikopesha katika Taasisi za kifedha zinazozingatia maudhui ya utu,ni furaha yangu kwamba tumefikia maakubaliano na mkopeshaji akakubali kurejesha milioni mbili kwa kila mhusika ,lakini ni muhimu watumishi wakajikopesha kwa tasisi zinazoeleweka ,nisingependa Mtu anastaafu anapata matatizo , alisema Gaguti.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akikabidhi kiasi cha Shilingi Milioni kumi kwa Mstaafu Mwl. Chrispin Christinian kwa niaba ya wastaafu wenzake wanne, pesa iliyorejeshwa toka Taasisi ya Mikopo ya Anny Credit Co.ltd
 
 
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini