Wafungwa wa KIKE Wafunguka Kuumia Kwa Kukosa Kufanya Mapenzi Wakiwa Gerezani | ZamotoHabari.



- Wafungwa huwa hawana nafasi ya kushiriki mapenzi gerezani na wanateta wapewe haki hio

- Wanawake kwenye gereza la Mtangani walisema wanaumia sana kwani wana hisia kama binadamu wengine

- Serikali imekuwa ikiteta kuwa haina vyumba vya kuruhusu wafungwa kujivinjari na wapenzi wao

Wafungwa wa kike wanaitaka serikali kutengeneza sheria itakayowaruhusu kushiriki tendo la ndoa wanapokuwa gerezani.

Wafungwa hao wanateta kuwa kiu cha kushiriki penzi kinawamaliza gerezani haswa wale wanaotumikia vifungo vya maisha na vile virefu.


Wafungwa wa kike wanataka serikali iwaruhusu kushiriki mapenzi gerezani. Picha: Nation
Wakiongea na K24, wafungwa hao walisema hali ni mbaya sana gerezani na wanaumia.

"Kupitia kwa mwongozo wa magereza humu nchini, serikali inafaa itengeneze sheria itakayowaruhusu wanawake wanaotumikia vifungwa virefu kufurahia tendo la ndoa na waume wao," Sofia Swaleh alisema.

Wafungwa hao walikuwa wakizungumza katika gereza la Mtangani kaunti ya Kilifi huku wakisema wanaumia sana.


Wafungwa gerezani huwa hawapati nafasi ya kushiriki mapenzi na wapendwa wao.

Msimamizi wa gereza hilo alisema ni kweli kina mama hawajakuwa na muda wa kumumunya tunda la penzi na waume wao kwani kwa sasa hilo halikubaliki.

Alisema ni lazima sheria iwekwe ili kuangalia mahitaji hayo ya kimwili kwa wafungwa.

Aidha hayo yanajiri wakati ambapo polisi wanachunguza kisa katika gereza la Kamiti mjini Naivasha ambapo inaarifiwa mfungwa aliwashambulia wenzake.


Gereza la Kamiti hukumbwa na visa vya wanaume kuonana kimwili.

Duru kwenye gereza hilo ziliarifu utata ulizuka kuhusu suala la mapenzi kati ya mfungwa huyo na wenzake wawili.

Mshambulizi anaarifiwa kukerwa na wawili hao kwa kuponyoka na mmoja wa mwenzao ambao inadaiwa alikuwa mpenzi wake.

Kwa upande wa serikali, wasimamizi wa magereza wamekuwa wakisema hakuna vyumba ambapo wafungwa wanaweza kupata nafasi ya kushiriki penzi na wapendwa wao.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini