Aslay Ataja Sababu zinazomfanya Mpaka Sasa Kuwa Single Baada ya Kuachana na Tessy | ZamotoHabari.

Aslay akiwa na mpenzi wake wa zamani
Msanii wa muziki, Aslay amedai kwa sasa hataki kukurupuka kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma.


Muimbaji huyo ambaye alikuwa kwenye mahusiano na Tessy na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja, amesema kwa sasa hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano.

“Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu Tessy ni ya mwanamke mwingine, ndio maana kwa sasa nipo single,” Aslay alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Aliongeza,
”Sitaki kukurupuka kutafuta mahusino mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa ni msanii na wengine wana tamaa”

Muimbaji huyo wiki hii ameachia wimbo wake mpya uitwao, Kwatu ambao umeonekana kupokewa vizuri na mashabiki wengi wa muziki nchini Tanzania.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini