Hali ya Uchumi ni Mbaya Rais Trump Hapakaliki.. Kushinikiza Kufunguliwa kwa Uchumi | ZamotoHabari.


Rais wa Marekani, Donald Trump leo anatarajia kutangaza mwongozo mpya wa kuufungua tena uchumi baada ya kufungwa kwa mwezi mmoja kutokana na mripuko wa virusi vya corona.

Hata hivyo, wataalamu wa afya, magavana na viongozi wa biashara wana hofu kuhusu kuibuka tena kwa visa vya corona bila ya kuwepo taratibu za itifaki zilizowekwa pamoja na kuwepo visa zaidi vya watu ambao hawajapimwa.

Trump alitangaza uamuzi wake wa kuyashinikiza majimbo kuondoa vizuizi vinavyowataka watu wabakie majumbani ambavyo viliwekwa mwezi uliopita ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona wakati ambapo idadi ya watu waliokufa Marekani ikiwa imefikia 31,000 hadi jana.

Trump anatarajiwa kufanya mkutano kwa njia ya simu na magavana wa taifa hilo baadae leo na kisha kuutangaza mpango wake katika mkutano na waandishi habari.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini