Mkali wa BongoFleva Harmonize, amefunguka masuala mawili ambayo ni kuhusu mke wake Sarah kuwa video vixen na kutotaka mke wake huyo kuzoeana na watu wengine au vyombo vya habari.
Ikumbukwe tu mke wake huyo alishoot naye kwenye video ya wimbo wake wa niteke, na haya ndiyo majibu yake endapo msanii mwingine atataka kumtumia kwenye video yake.
"Mke wangu sio video vixen, ali-shoot video na mimi kwa sababu ni mume wake, hata mimi siwezi kufanya naye kazi hiyo tena, maana nikifanya hivyo itakuwa nimemuhalalisha kwamba video vixen ni kazi yake" amesema Harmonize.
Pia akizungumzia juu ya kutotaka mke wake huyo kutozoeana na watu, wasanii wengine na vyombo vya habari Harmonize amesema "Nilitamani iwe hivyo ila sio kama nimeweka hatakiwi kufanya hivyo, kwa sababu tayari ameshakuwa maarufu, watu wanamuona na kumfuatilia ila natamani ingekuwa hivyo japo najua haiwezekani".
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments