Kenya Yasema Wagonjwa 3 Wapya Walitokea Tanzania | ZamotoHabari.



Idadi ya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 184, baada ya visa vipya vitano kuthibitishwa hii leo, ambapo watatu ni raia wa Kenya na walikuwa wamesafiri kutokea Tanzania na wawili walisafiri kutoka Uingereza na Nchi za Falme za Kiarabu.


Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 9, 2020, na Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe, wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya Corona nchini humo.

"Kwa masaa 24 yaliyopita tumepima sampuli za watu 308 na kati ya hao watano tu ndiyo wamekutwa na COVID-19, watatu ni Wakenya waliokuwa wamesafiri kutokea nchini Tanzania na wawili kutoka Uingereza na Nchi za Falme za Kiarabu" amesema Mutahi Kagwe.

Aidha Idadi ya vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona nchini humo imeongezeka na kufikia vifo 7, baada ya hii leo tena kuthibitisha kifo cha mtu mmoja.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini