Kigwangalla: Kutumbuliwa Siyo Shida Kwangu, Nishachoka! | ZamotoHabari.


KUFUATIA Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2019 kubaini matumizi ya Sh 2.58 bilioni yaliyofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii nje ya bajeti na kabla ya kupitishwa na Bunge, waziri mwenye dhamana ameajitosa na kuamua kujibu tuhuma hizo.

Akitoa ripoti hiyo, pamoja na mambo mengine mengi, CAG, Charles Kichere alisema, “Nilipitia matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kubaini kiasi cha Sh 2.58 bilioni kimetumika kufanikisha kampeni ya Urithi Festival Celebration and chaneli ya Televisioni maalum “Urithi Festival” ya kutangaza vivutio vya utalii kinyume na taratibu.”

Ripoti hiyo ilienda mbele zaidi na kusema fedha hizo zilitolewa katika vifungu vingine vya matumizi ya wizara na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ambazo ni Tanapa, NCAA, Tawa na TFSA na hayakufuata utaratibu.

“Nilijulishwa kuwa bajeti ya Urithi Festival ilipitishwa na menejimenti ya Wizara katika vikao mbalimbali vilivyofanyika,” inaeleza taarifa hiyo.

Baada ya ripoti hiyo kutoka, baadhi ya wafuasi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakiandika maoni yao mitandaoni na kumtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakimtaka aweke bayana kuhusu sakata hilo, huku baadhi yao wakimtaka awajibike na wengine wakimpongeza kwa kufanya kazi nzuri na kuanzisha Channel maalum itakayotangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Naye Waziri Kigwangalla hakukaa kimya, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameamua kujibu hoja na moja ya mambo aliyosema ni kwama amesema;
 “Kutumbuliwa siyo shida sana kwangu, maana hata mimi nishachoka kujitoa kuwatumikia watu wasio na shukran kama wewe! Unadhani kuwa Waziri ni feva kwangu ama ni fursa kubwa sana kwangu, hiyo ndiyo shida. Kwangu ni nafasi ya utumishi na ninajitoa sana kuitumikia nchi yangu.”


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini