Mjue Mnyama NGEKEWA , Mnyama Anayeongoza Kwa Kupendwa na Wanyama Wengi Duniani | ZamotoHabari.



Huyu ndiye mnyama anayeongoza kupendwa na wanyama wengi zaidi duniani, anapokaa huzungukwa na viumbe wengi tofauti kiurafiki. Hupatikana zaidi Marekani Kusini na Kati

Analiwa na wanyama wachache sana, haswa aina fulani ya mamba ‘caiman’, chui aina ya ‘Ocelot’, jagwa, puma, tai na nyoka wakubwa kama Anaconda. Adui yake mkubwa zaidi ni binadamu ambaye humla na kutumia ngozi yake kwa sababu za kiimani

Huyu ni mnyama jamii ya sungura, anaweza kufikia Kg 75 akiwa mkubwa, na urefu wa mita 1.4. Ana uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 5. Maisha yake ni maeneo yenye majani mengi yaliyo karibu na maji

Anaishi kwa kula majani yaliyo nchi kavu, yaliyo ndani ya maji na viumbe wa baharini kama majani yakiadimika. -
Ngekewa asubuhi hula kinyesi chake ili kupata ‘virutubisho’.

Iliaminika mtu akiwa na kipande cha ngozi ya mnyama huyo anakuwa anapendwa na wengi, ndio sababu wanaopendwa huambiwa 'una ngekewa'

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini