Mwanamke mmoja aliyewekwa kwenye karantini ya jijini Dar es Salaam ametoroka na kukamatwa na jeshi la polisi akiwa mkoani Iringa.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuwa kuna mtu mmoja ametoroka kwenye karantini na anaonekana mkoani Iringa.
“Tulichokifanya tukashirikiana na jeshi la polisi tunashukuru sana tumefanya kazi vizuri tukapata location yake tukapata nyumba aliyokuwa amekaa tukaongea na mganga mkuu wetu tukamfuata na kumpeleka katika karantini yetu ambayo tumeitinga hapa,” amesema
Kasesela amesema mwanamke huyo ameingia Tanzania ana siku ya nne akiwa anatokea Norway alivyowekwa karantini siku ya tatu akaamua kutoroka.
“Kuna dalili ambazo sio nzuri zinasemekana watu kutoroka katika karantini kuna mwingine nimesikia ametoroka wiki iliyopita sijui katimkia wapi ni vizuri unapowekwa karantini uzingatie na sio kutoroka,” alisema Kasesela
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments