NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE NCHINI CHINA AFAFANUA SABABU ZA KUBAGULIWA KWA BAADHI YA WAAFRIKA NCHINI HUMO | ZamotoHabari.


Mabalozi wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China China Mhe. CHEN Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa Mataifa ya Afrika katika Mji wa Guangzhou uliopo katika Jimbo la Guangdong.




Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NAIBU Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa China Chen Xiaoding amekutana na mabalozi wa nchi za Afrika akiwemo balozi wa Tanzania nchini humo Mbelwa Kairuki na kufafanua taarifa na changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa mataifa ya Afrika katika mji wa
Guangzhou uliopo katika jimbo la Guangdong.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema kuwa Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa si sera ya China kuridhia masuala ya ubaguzi kwa namna yoyote ile na kueleza kuwa China ni rafiki wa kweli na wa majira yote kwa Tanzania na mataifa yote ya Afrika.

Mbelwa amesema, Serikali ya China imeeleza kwamba haiwezi kukubali vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kudharirisha utu wa mtu yeyote yule.

Aidha amesema kuwa Naibu Waziri huyo ametoa maelezo ya masuala yanayoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na waafrika kupimwa Covid -19 kwa lazima na kubaguliwa kwa waafrika waishio katika jimbo la Guangdong.

Kuhusiana na waafrika waliopo katika Mji wa Guangzhou kulazimishwa kupimwa Covid-19 kwa lazima, Naibu waziri amesema kuwa;
 "Serikali ya Jimbo la Guangdong ilibaini kuwa wageni waliokuja kutoka nje kuja katika jimbo la Guangdong kati ya watu 26 waliokutwa na maambukizi watu 19 walikuwa wametokea Afrika na ni Waafrika" ameeleza Kairuki.

Pia amesema jambo jingine lililopelekea waafrika kupimwa kwa lazima ni baada ya watu 60 ambao hawakuonesha dalili licha ya kuwa na virusi nwatu 57 walikuwa waafrika  na katika jimbo hilo la Guangdong visa vipya 15 vya ndani vilivyoripotiwa kesi 13 ni za watu wa Afrika.

 CHEN Xiaoding ameeleza kuwa sababu hizo zimepelekea  kupima Covid-19 kwa lazima na walichokiri ni kutotoa taarifa mapema na  baadhi ya watoa huduma kutokuwa na staha jambo ambalo Naibu Waziri amekiri mapungufu kwa baadhi ya watendaji katika utekelezaji wa zoezi hilo.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini