Nuh Mziwanda "Nimepoteza Vitu Vingi Sana Sababu ya Mapenzi" | ZamotoHabari.


Mkali aliyetamba na wimbo wa "jike shupa"  Nuh Mziwanda amesema ameumizwa na ameteseka sana kwenye mapenzi hali ambayo imempelekea kupoteza vitu vingi kama familia na mashabiki zake.


Nuh Mziwanda ameweka wazi hilo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa, anajaribu kusahau yote yaliyopita japo kuna mtu mmoja anamfuatilia sana kwenye maisha yake.

"Nimeumizwa sana na mapenzi, yamenitesa sana mapenzi, nimepoteza vitu vingi sababu ya mapenzi, mashabiki  na familia yangu nimewachanganya sana akili, nikakaa muda mwingi bila ya kuwa na mahusiano makini kujaribu kusahau yote niliyopitia  kuna kidudu mtu bado ananifatilia  japo tayari ana maisha yake na yanamtosheleza, niache na roho yangu mama inatosha" ameandika Nuh Mziwanda


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini