Katavi. Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linatarajia kumfikisha mahakamani raia mmoja wa China Lin Guosong (34) mfanyabiashara wa Majengo Sumbawanga akituhumiwa kukiuka amri halali iliyowekwa na Serikali ya kunawa mikono kujikinga na corona.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Aprili 11,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamini Kuzaga amesema mtuhumiwa amekiuka utaratibu huo Aprili 5, 2020 katika kizuizi cha Ntibili Majimoto.
"Mtuhumiwa alikuwa anaendesha gari lenye namba za usajili... akiwa na msaidizi wake James Mpepo (28)mkazi wa Bomani Sumbawanga, baada ya kufika eneo hilo mwenzake alishuka na kutii amri ya kunawa lakini yeye alikaidi," amesema Kuzaga.
Kuzaga amesema Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ntibili, Josephat Mgelwa alitoa taarifa kituo cha polisi Majimoto ambapo polisi walifika eneo hilo na kumkamata mtuhumiwa.
"Baada ya kumhoji hakuwa na maelezo yoyote, pia mwezake alimsihi kushuka ili anawe alikataa bila kuwa na sababu za msingi, polisi walichukua hati yake ya kusafiria Na.E09809632, na muda wowote tutamfikisha mahakamani baada ya sikukuu,"
Mwananchi
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments