Sababu ya Nedy Kufuta Picha Instagram, Amtaja Ommy Dimpoz | ZamotoHabari.



Msanii wa Bongo Fleva, Nedy Music ametaja sababu iliyopelekea kufuta picha zote katika mtandao wa Instagram na kuamua kutotumia mtandao huo kwa muda wa mwezi mmoja.

Akipiga stori na Friday Night Live (FNL) ya EATV, Nedy amesema kuwa aliamua kufuta picha zote na kutotumia mtandao huo kwa mwezi mmoja ili kuweka mikakati yake sawa kwa ajili ya ngoma yake mpya aliyoitoa hivi karibuni.

"Siyo kufuta baadhi ya picha, niliamua kufuta picha zote Instagram na kukaa bila kutumia mtandao huo kwa mwezi mmoja, nilikuwa napanga mkakati wangu sawa kwa ajili ya wimbo wangu mpya", amesema Nedy.

Kuhusu kutoelewana na mtu wake wa karibu na aliyekuwa meneja wake Ommy Dimpoz chini ya 'lebel' ya PKP, Nedy amesema, "kwanza niweke wazi sina ugomvi na Ommy Dimpoz, ni mtu ambaye amenisapoti mpaka hapa nilipofikia leo na nitaendelea kumtumia katika muziki wangu".

"Yeye kutoposti kazi yangu haimaanishi kwamba hanisaidii, mimi naamini yeye anajivunia kuona mimi niko sehemu fulani na hicho ndicho kitu kikubwa sana", ameongeza Nedy.

Nedy ametoa wimbo mpya hivi karibuni unaojulikana kama 'Amen' ambao mpaka sasa una watazamaji taktibani 170,000 katika mtandao wa YouTube

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini