TANDAHIMBA KUVUNA ZAIDI YA TANI MIA NANE YA ZAO LA UFUTA KWA MSIMU HUU, | ZamotoHabari.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema wanatarajia kupata zaidi ya tani Mia nane ya zao la ufuta kwa msimu huu 2020

Ameyasema hayo alipotembelea shamba la mkulima  Hassan Chipyangu (udede) ambalo lipo katika kata ya Michenjele

"Msimu huu tunatarajia kupata zaidi zao la ufuta baada ya mwitikio wa  wakulima kulima zao hilo hapo awali wakulima walielekeza nguvu zao kwenye zao mo ja lakini Sasa wanafunguka kwa kulima mazao mengine,"amesema Waryuba

Aidha amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo Cha ufuta kwani kimeonekana  kustawi katika Wilaya hiyo badala ya kutegemea zao la korosho pekee

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka  amesema walitenga  kiasi Cha Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya mbegu ambazo walipewa wakulima kwa makubaliano kuwa wakivuna warudishe mbegu hizo ili wapewe na wengine  

"Kwa Hali ambayo naiona katika mashamba mengi ya ufuta tuliyoyatembelea ndani ya Hamashauri,ufuta umeonekana kustawi hivyo  ili uzalishaji uendelee kuwa wa viwango vikubwa  tunatarajia kuanza kuwashindanisha maafisa ugani wa kata zote za Halmashauri,"amesema Msomoka

Hata hivyo amesema watawashawishi wananchi katika mfuko wa fedha za akina mama,vijana na walemavu kulima zao la ufuta badala ya kubuni miradi ambayo badae inawashinda kurejesha fedha hizo kwa wakati
 Dc Waryuba (kulia)akiwa na Mkurugenzi Said Msomoka (kushoto) walipotembelea shamba ekari 10 la mkulima Udede
Shamba la mfano lililopo Kijiji Cha Michenjele Wilaya ya Tandahimba


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini