Wakenya Wakamatwa Tanzania na Kupelekwa Karantini | ZamotoHabari.


Watu wanne kutoka nchini Kenya wamekamatwa na kupelekwa karantini baada ya kuingia nchini kwa njia za panya.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu leo Aprili 14, 2020 amesema kuwa kutokana na nasaba za pande mbili watu wanapenya kutoka Kenya kwa njia za panya na kuingia kwa ndugu zao ambao hukaa kimya bila kutoa taarifa.

“Tumekamata watu wanne tumewaweka kwenye kituo chetu cha karantini shule ya watu wenye ulemavu, wengine wanasiku saba wengine siku tano wanapimwa kila siku asubuhi na jioni wanapimwa hali zao daktari,” amesema.

Amesema wanapopita Tarime hawasemi wanaenda wapi lakini baadae wanapenya hadi Serengeti na wameweka watu ambao wanawasaidia kuwabaini.

“Viongozi wa vijiji na kata tumewapa majukumu ya kubaini watu wote wanaoingia kinyamera il mamlaka ziweze kuchukua hatua, huku kuna mwingiliano mkubwa wa makabila lazima tuwe makini hasa kwa wanaopita njia za panya,” amesema.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini