Na Shukrani Kawogo-Michuzi TV, Njombe.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wilayani Ludewa Mkoani Njombe ikiwemo nafasi ya ubunge wametakiwa kuacha kuchafuana na kufanya kampeni kabla ya nafasi hizo kutangazwa kuwa wazi kwani kwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kukatwa majina yao .
Hayo aliyasema katibu wa chama hicho wilayani humo Bakari Mfaume na kuongeza kuwa kumekuwa na matamanio kwa baadhi ya wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama ya ubunge na udiwani na kupelekea kuchafuana ili kujipatia sifa na kuwashawishi wapiga kura.
Alisema kuwa watia nia hao wanapiga kampeni za chini chini wakidhani kuwa katibu huyo hapati taarifa zao kwakuwa yupo eneo tofauti na wanaloenda wao kitu ambacho si cha kweli kwakuwa katika kila maeneo kuna watendaji wa chama hivyo yanapotokea mambo kama hayo anapata taarifa kupitia watendaji hao.
“Watu wamekuwa wakidhani kuwa kuna uvunjifu wa kanuni lakini mimi nimenyamaza kitu ambacho si cha kweli kwakuwa katibu ni taasisi unaweza ukaniona nipo eneo tofauti na alilopo mtia nia lakini ninapata taarifa za kila mtu na mambo anayoyafanya kwakuwa huko nako kunaviongozi wa chama”, Alisema Mfaume.
Aliongeza kuwa wanachama wanaohitaji kugombea nafasi hizo wanapaswa kufuata kanuni na taratibu kwani endapo wataenda kinyume watakuwa wamepoteza sifa ya kugombea na muda wa kugombea utakapofika wasishangae kuona majina yao yamekatwa .
Alisema mpaka sasa wameshapokea kesi moja ambapo waliifikisha katika kamati ya usalama na maadili kisha ikafikishwa katika kamati ya siasa kwa ajili ya kufanya maamuzi na endapo itabainika wahusika kuwa wanahatia basi watakuwa wamepoteza rasmi sifa ya kugombea.
Katika hatua nyingine katibu huyo amesema kuwa katika upande wa wilaya hiyo ilani ya chama imetekelezwa kwa asilimia kubwa kwani kwa kipindi cha miaka mitano wameweza kupunguza tatizo la maji katika baadhi ya maeneo, zahanati, ufaulu wa wanafunzi pamoja na miundombinu ya barabara.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Bakari Mfaume

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments