Waziri Mohamed: Sio sheria kutaja majina na wasifu wa mgonjwa wa Corona | ZamotoHabari.


Waziri wa afya wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, amesema ni kinyume cha sheria kutaja majina na wasifu wa wagonjwa walioathirika na virusi vyake Corona.

Waziri amewataka wananchi kutekeleza njia za kujikinga na maradhi hayo na sio kujua ni nani ambaye ameathirika.

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Dalili za Corona ni zipi?

Dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu.

Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Lakini isikutishe, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

Makundi yaliyo kwenye hatari zaidi ni yapi?

WHO inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini