Wema Sepetu "EX wangu Alikihusudu Kipara Changu ila Nilijilipua Sana Aisee" | ZamotoHabari.



Leo  Alhamisi Aprili 9,2020, watu wengi ifikapo siku hii kujikumbushia matukio ya zamani yaliyopita kuanzia picha, video na simulizi siku hii huitwa "TBT".

Kupitia ukurasa wa Instagram anaoutumia staa wa filamu hapa nchini Wema Sepetu, amekumbushia tukio lake la kunyoa kipara, huku akieleza kuwa mpenzi wake wa zamani aliipenda style hiyo.

Kwenye post hiyo Wema Sepetu ameandika kuwa  "ThrowBack Thursday, ila kama ni kuthubutu jamani nilijuaga kuthubutu kwa kweli, para kama ngozi halafu nilikuwa naingia popote, muda wowote ninavyotaka hata nikioga nasikia raha, halafu wakati huo aliyekua mpenzi wangu akawa anakihusudu kipara pia, basi mambo yakawa bulbul, maisha haya" ameandika Wema Sepetu.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini