Yanga Wasema Wanatamani LIGI imalizike Bingwa Apatikane Kihalali | ZamotoHabari.




Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga SC wamesema wanatamani kuona janga la Corona linaisha ili ligi iendelee ili bingwa apatikane kama ilivyo ada.

Yanga wametoa taarifa ya kueleza msimamo wao leo Aprili 3, 2020 kuatiwa taarifa zilizoenea kuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo amesema ligi msimu huu ifutwe na ubingwa wapewe watani wao Simba.

“Taarifa zilizotolewa na majo ya magazeti ya michezo na kunukuliwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli kwani Makamu mwenyekiti Fredrick Mwakalebela alitoa maoni tofauti na yaliyonukuliwa,” inasema taarifa hiyo ya Yanga.

Itakubukwa kuwa katika msimamo wa ligi hiyo ambayo hivi sasa imesimama sababu ya mlipuko wa corona Yanga iko nafasi ya tatu huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na inahitaji pointi 12 pekee ili itangazwe bingwa hata kama ligi

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini