JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA LATOA ONYO KWA WAVURUGA AMANI PAMOJA NA MADEREVA WALEVI NA WASIOZINGATIA SHERIA | ZamotoHabari.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limetoa onyo kwa watu wachache wanaopenda kuvuruga amani katika kipindi cha sikukuu na kuwataka waache mara moja kuwa na fikra hizo kwani watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza Kamanda wa polisi mkoani hapa Jonathan Shana amesema kuwa kwa upande wa madereva wa vyombo vya usafiri ni marufuku kuendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa ,mwendokasi pamoja na kujaza abiria kupita kiasi kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
Aidha Jeshi hilo limewashukuru wananchi kwa wote mkoani hapa kwa ushirikiano na utulivu wanaoendelea kuuonyesha katika kipindi chote cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao ni nguzo muhimu katika dini ya kiislamu.

Amesema katika kuhakikisha kuwa wanasheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu kwani jeshi hilo limejipanga vyema katika kuhakikisha sikukuu hiyo ninafanyika kwa amani na utulivu.

''Mara nyingi baada ya mfungo huo mtukufu waumini wa dini ya kiislamu watasheherekea sikukuu ya Eid el Fitri ambapo kwa mwaka huu itakuwa kati ya tarehe 24/5/2020 au 25/5/2010 tumejipanga kuhakikisha wanasheherekea kwa amani na utulivu'' alisema kamanda Shana
Kamanda Shana ametoa wito kwa wananchi kila mmoja na nafsi yake kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam waAfya kuhusu ugonjwa wa corona COVID-19 ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Jeshi la polisi mkoani Arusha limewatakia wananchi wote sikukuu njema ya Eid el Fitri.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini