Jinai za Trump Dhidi ya Watu wa Palestina Hazina Mfano wake Katika Historia | ZamotoHabari.


Mbunge wa Tunisia amesema kuwa jinai za Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya raia wa Palestina hazijawahi kushuhudiwa katika historia.

Zuhair Hamdi aliyasema hayo Alkhamisi ya jana na kuongeza kwamba, jinai za Trump kuhusiana na haki ya raia madhlumu wa Palestina hazijawahi kushuhudiwa tena katika historia na kwamba, rais huyo wa Marekani amefanya jinai kubwa dhidi ya taifa la Palestina na haki zake. Hamdi ameashiria pia juhudi za baadhi ya nchi za Kiarabu za kuboresha uhusiano na Wazayuni maghasibu na kubainisha kwamba raia wa nchi hizo wanapasa kukabilina na juhudi hizo za kufanya uhusiano na utawala huo bandia wa Kizayuni kuwa wa kawaida.

Zuhair Hamdi amesema kwamba hiyo ndio njia pekee ya kistratijia ya kuelekea kwenye ukombozi na umoja. Mbunge huyo ambaye ni kiongozi wa chama cha Popular Movement nchini Tunisia ameongeza kwamba mataifa na nchi za Kiislamu zina majukumu kuhusiana na kadhia ya Palestina na kwamba ni lazima ziwe pamoja na raia wa taifa hilo madhlumu.



Hamdi ameelezea pia suala la kuainishwa na Imam Khomeini (MA) Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, na kusema kwamba hatua hiyo ina nafasi muhimu katika kuimarisha utamaduni wa muqawama na kujitolea kwa walimwengu. Hatua ya baadhi ya tawala za Kiarabu ya kuboresha uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni inajiri katika hali ambayo kwa miaka mingi utawala huo mbali na kufanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya Wapalestina, pia umeyakalia kwa mabavu maeneo mengi ya Kiarabu na Kiislamu.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini