WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kikiwa kwenye mpasuko baada ya baadhi ya wabunge wake kukaidi agizo la Chama hicho kuwataka kutohudhuria Bunge na kisha kukaa 14 kama sehemu ya kujilinda na virusi vya Corona limechukua sura mpya baada ya Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya Chama hicho Peter Lijualikali kuelezea hatua kwa hatua madhara ya Lockdown kwa Watanzania na namna ambavyo aliamua kutokubaliana na uamuzi huo kwa maslahi ya wananchi.
Akizungumza zaidi mbele ya waandishi wa habari , Mbunge Lijualikali amesema kwa kina mbele ya waandishi mtifuano ndani ya Chadema umetokana na ishu ya Corona na kwamba walisema lazima waende Bungeni kwasababu hakuna hoja ya wao kususia Bunge na hoja hiyo haikuwa haikuwa shirikishi ndio maana aliamua kuingia kwenye vikao vya Bunge.
"Msimamo wa Chama changu tuwe na Lockdown kwa maana ya Corona , nataka kuwaambia watu wa Kilombero, Ifakara na Watanzania hebu tujiulize kwa mazingira yetu ya Tanzania tukiwa sober kabisa , kwa mfano pale Ifaraka tuweke Lockdown , kwamba wafanyabiashara wa Dar es Salaam wasiende kununua mpunga na watu wa Ifakara wanafanya kazi ya kilimo ya mpunga kwasababu kwani ndio biashara kubwa.
Wakulima wanalima ili wauze, kama hakuna uuzaji, Ifakara imefungwa hivi wataishije."Pale Ifakara sokoni, watu wote wale uwaambie biashara ifungwe kwasababu ya Corona hivi wataishije? Yaani watu wa Kilombero mnataka kuwaambia ndio wazo langu hilo , ningekuja kuwauliza eti Kilombero tuweke Lockdown au tusiweke, mngenipiga mawe na huu ni ukweli, hili tulilikataa kwamba hii sio aproach nzuri , kwa uchumi wetu sisi hili ni tatizo mimi watu wangu kule unawezaje kuwaambia wawe Lockdown , yaani mimi naanzaje, watu wanatakwenda shambani kung'olea mpunga, watu wanataka kwenda kuvuna uwaambia kaeni ndani, msitoke nje kuna corona.
"Yaani mimi nikuhukumiwe kwasababu hii , halafu hebu tuulize hivi watu wanampiga Rais Dk.John Magufuli eti hapendi watu, hivi kweli Rais Maguguli afanye maamuzi ambayo yatua Watanzania kama kule Itali, Marekani au kama china.Yaani Rais wa nchi ambaye ameapa kulinda wananchi wake, ameapa kuilinda Katiba afanye maamuzi ambayo yatauaa watanzania.Maamuzi ambayo,watu wanakufa 700, 800 kwa siku , 900 au 1000, Rais wa nchi , hivi Rais Magufuli yeye hiyo inamsaidieaje? Anapata faida gani ?
"Yeye kama Rais wa nchi anasikia raha gani watu wanakufa hivyo kwa huo wingi, mpaka aamue kitu ambacho muundo mzima wa vyombo vya usalama wa nchi ukae kimya.Sijaona mimi pale mshemiwa anasema nafunga maduka yote haya, sijaona, watu wafunge hoteli kwasababu ya Corona sijaona , kwa hiyo sisi masikini tukae ndani lakini wao ofisi zao na hoteli zao hawafungi.
"Sasa kama hawafungi ofisi zao nani anakwenda kuhudumiwa kama sio sisi , usanii tu.Hakuna namna yoyote ambayo Rais Magufuli atapata faida yoyote akiona watu wanakufa kwasababu ya Corona... hakuna na kwasababu hiyo hawezi kufanya maamuzi anayoona watu wanakwenda kufa, hawezi tuache propaganda za kijinga, na hii ni tabia yao .
"Ndio Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Peter Msigwa(Mbunge wa Iringa Mjini) anaomba radhi sasa hivi kwamba jamani ee Mzee Kinana anisamehe nilidaganya watu na watu wanamuamini. Ameongelea bungeni sehemu ambayo tunatakiwa kuongea ukweli yeye anaongopa na leo anaomba msamaha. Tena alitumia neno gumu sana, amefanya vile kwasababu za kisiasa na kizandiki, alisema uongo kwasababu za kisiasa na kizandiki.Kwa hiyo yeye anaongea kwasababu za kisiasa na kizandiki.
"Siasa ya aina hiyo kwa ajili ya nini?Msaidie yeye na Chama chake dhidi ya Chama cha CCM na Serikali yao, yaani ni sababu ndogo, haitaji mtu asome sana , ni elimu ndogo tu.Halafu huyo ndio Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema anakaa na Mwamba(Freeman Mbowe), halafu mimi ni baki chama hiki.Tuwe makini sana na watu hawa walaghai, nchi inatakiwa kwenda mbele, inatakiwa isonge.Hata hivyo ieleweke sijahamia CCM ila nimeomba kuhamia CCM,na kama wataniona sifai basi nitaenda kulima mpunga lakini Chadema sirudi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments