Nenda kwa mwendo wako,mafanikio sio mashindano, kila mmoja atafanikiwa kwa muda wake-Dina Marios



Hili neno hata mimi huwa naishi nalo.Kwenye maisha yangu huwa nafanya juhudi kujiboresha mimi.Mimi wa juzi na jana basi leo niwe bora zaidi ya juzi na jana.


Hata wakiinuka watu kutaka kushindana na mimi huwa nawaangalia tu wanavyojichosha.Kubwa nawaonaga kama changamoto ambayo imekuja kunipa kasi zaidi ya kuendelea kujiboresha.
Jitambue,Jikubali,jiboreshe,jiimarishe, kimbia mbio zako wewe ndio unajua unachokitaka na unachokitafuta.Dunia ni pana sana na ina FURSA kwa kila mmoja wetu nyingine bado hata hazijagunduliwa kazi ni kwako tu kuzing'amua.
Dina Marios

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini