DAR: Video vixen wa Wimbo wa Bedroom wa mwanamuziki Rajab Abdul ‘Harmonize’, Nicole Mbaga amesema umaarufu ni mzigo baada ya kushukiwa amebeba madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar.
Nicole ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, hakutegemea kabisa kama anaweza akakutana na changamoto kama hiyo maishani mwake, kwani alijikuta akipekuliwa kwa dakika 30 kisha kupigishwa push up akiwa hapo airport.
Nicole anasema ishu hiyo ilimfanya kuchanganyikiwa kujiuliza kwa nini inakuwa hivyo wakati yeye ni kama wasafiri wengine.
“Kiukweli ilikuwa ni safari yangu ya kwanza kukutana na changamoto kama hiyo.
“Nilikuwa siwezi kupiga push up, lakini nikaweza ili tu nijinusuru na sikuelewa kwa nini ilitokea hivyo,” anasema Nicole.
Nicole aliendelea kusema kuwa, baada ya kumuona ni msichana mdogo, lakini ana pesa nyingi na amevalia vito vya dhahabu, hilo ndilo lilikuwa kosa kwake, kwani askari wa Airport waliamua kumuweka kando na kuanza kumpekua kila kitu hadi nguo zake zote alizobeba, jambo ambalo anasema lilimfedhehesha mno.
“Hivi jamani kweli mimi siwezi kumiliki pesa nyingi kwenye pochi yangu? Au kuvaa vito vya dhahabu ni kosa? Yaani walinipekuwa vya kutosha mpaka waliporidhika ndipo wakatulia, tena baada ya kunihenyesha kwa takriban dakika zaidi ya 30,” anasema Nicole ambaye hivi karibuni alitrendi baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na Harmonize.
Mrembo huyo alizidi kufunguka kuwa, tangu zamani alikuwa hapendi kabisa mambo ya umaarufu maana yatamfanya ashindwe kuendelea na mambo mengine kutokana na macho ya watu.
“Nilikuwa ninaenda sokoni Mwenge (Dar) nikiwa nimesuka zangu nywele nzuri za kwenda nyuma, nilikuwa ninatembea na hakuna mtu wa kuniangalia au hata kuniuliza kitu, lakini sasa hivi nashindwa,” amesema.
Nicole alianza kujizolea umaarufu kwa kasi baada ya umbo lake kuonekana la tofauti kutokana na jinsi alivyoumbika utadhani amechongwa pamoja na vitu anavyomiliki ambavyo haviendani na umri wake.
OPEN IN BROWSER
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments