Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na misukosuko ya maisha, ukosefu wa chakula, magonjwa na kipato inaelezwa kuwa ndiyo sababu ya bara la Afrika kuwa la mwisho kwenye orodha ya nchi zenye wanaume ambao wanawaridhisha wake zao kwenye ndoa wakiwa faragha.
Kwa utafiti uliofanywa na mtaalamu wa masuala ya ya mahusiano an aliyebobea kwenye masuala ya ndoa, Bi Victoria Milan kupitia mtandao wake wa victoriamilan.com unaojihusisha na masuluhisho, ushauri na takwimu mbalimbali za mahusiano mtafiti huyo amesema nchi za Ulaya, ndiyo zinaongoza kwa wanaume kuwaridhisha wake zao kwenye ndoa ukilinganisha na mabara mengine kama Amerika, Asia na Afrika.
Bi Milan amesema kwenye utafiti huo alitumika idadi ya watu 9,165 walio kwenye ndoa kutoka nchi 80 za mabara ya Afrika, Ulaya, Asia na Amerika ya Kusini/Kaskazini ambapo kila nchi alihoji ndoa 80 hadi 82 kutokana na idadi ya watu wa nchi husika.
Kwenye takwimu hizo alipata wastani wa muda wa wapenzi wanaotumia wakiwa faragha kwa kila mzunguuko mmoja ambapo wastani wa nchi za Ulaya ulikuwa ni dakika 32.1 kwa kila mzunguumko mmoja wa tendo la ndoa ambapo nchi zilizoongoza ni Denmark, Finland na Sweden.
Bara lingine ambalo limefuatia ni Amerika ya Kaskazini/Kusini ambapo wastani wao ni dakika 23.4 wakiongozwa na nchi za Marekani na Canada.
Bara la tatu ni Asia na la mwisho kwenye utafiti huo ni Afrika ambapo wapenzi walio kwenye ndoa hutumia wastani wa dakika 5 kwa mzunguuko mmoja na nchi zinazoongoza kwa kukaa muda mrefu kwa mzunguuko mmoja ni Nigeria na Afrika Kusini.
Orodha ya nchi hizo ni kama ifuatavyo NB: Huu ni muda ambao wanaume hutumia kwa kila mzunguuko mmoja bila ya maandalizi.
1- Denmark Dk 43
2-Marekani Dk 41
3- Finland Dk 39
4- Canada Dk 36
5- Norway Dk 34
6- Uingereza Dk 33
7- Ujerumani dk 31
8- Czech Republi Dk 29
9- Ireland Dk 27
10- Austria Dk 27
Kwenye orodha hiyo ya 10 bora duniani hakuna hata nchi moja kutoka Afrika ingawaje nchi ya Nigeria imeingia kwenye 20 bora kwa kushika nafasi ya 19 ikiwa nawastani wa dakika 20 ikifuatiwa na Afrika Kusini nafasi ya 20 ikiwa na Wastani wa dakika 18 pekee.
Sababu kubwa zilizotajwa kwa wanaume wengi kwenye ndoa kutumia muda mfupi kwenye tendo hilo ni uvivu, Mazoea, majukumu ya kila siku, msongo wa mawazo na aina ya vyakula .
“Wakati nafaya utafiti wanandoa wengi hususani wanawake walisema kabla ya ndoa wenza wao walikuwa wakitumia muda mwingi kuwaandaa na hata kwenye tendo lenyewe lakini baada ya kuishi nao walianza kupoteza uwezo wao kitandao”,amesema Bi Milan kwenye mdahalo wa kipindi cha Loose Women kinachorushwa na kituo cha itv cha Uingereza .
Hata hivyo kwenye utafiti huo amebaini kuwa Wanawake ambao wanaridhishwa na wenza wao bado wanaonekana ni vijana wenye afya na nyuso zenye furaha ukilinganisha na wale ambao hawaridhishwi kwenye tendo la ndoa.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments