· NI SEHEMU YA MPANGO WA KUSAIDIA JAMII KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
Tarehe 24, Mei 2020, Zanzibar QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza yenye asili ya Asia imetoa msaada wa magunia ya vyakula, galoni za mafuta ya kupikia, vifaa vya usafi, vinywaji baridi na vitakasa mikono (sanitizers) kwenye nyumba ya kulelea yatima ya Mazizini Zanzibar. Hizi ni jitihada za mwezi mtukufu wa ramadhani zenye lengo la kuboresha maisha ya walio wengi na inaendana na falsafa ya kampuni ya QNET ya ‘Raise Yourself to Help Mankind’ (RYTHM).
Huu unakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo kampuni ya QNET imetekeleza jitihada zake za kurudisha mapato yake kwa jamii inayoizunguka (CSR) katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Tanzania. Katika miaka iliyopita, misaada kama hii ikiwepo misaada ya kufedha ilitolewa kwenye vituo vya yatima katika maeneo ya Dar es salaam na Dodoma.
Katika mwaka huu, msaada wa aina hii umetolewa katika zaidi ya nchi 15 duniani kote ikiwemo Kenya, Ivory Cost, Mali, Cameroon na Tanzania katika bara la Afrika, na jambo hili linaakisi madhumuni ya kampuni ya QNET kuleta manufaa katika jamii ambako inaendesha shughuli zake.
Akipokea msaada huu kwa niaba ya kituo hico, Naibu Wizara wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanazibar Shadia Mohamed, alitoa shukurani zake na kuwasii mashirika na taasisi zingine kuiga mfano huu hasa sasa wakati nchi inapambana na ugonjwa wa Corona.
“Nashukuru kampuni ya QNET na ninahamasisha makampuni na mashirika mengine kuiga mfano huo wa kufanya vitendo vya wema na ukarimu”.
Akitoa maoni kuhusu tukio hilo kwa mwaka huu, Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall amesema,"Msaada katika kipindi cha Ramadhani imekuwa ni moja ya kampeni zetu kubwa kila mwaka. Kwa kweli imekuwa ni jambo la maana, lenye kugusa moyo na kupendeza kwa kampuni ya QNET Kampeni kama hizi zinakuza uwezeshaji kwa jamii na vile vile zinahamasa sana kwa wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu wa Kujitegemea. (Independent Representatives.)".
Naibu Waziri Wizara wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed (kushoto), akipokea msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 5, 462, 000 kutoka kwa mwakilishi wa (RYTHM FOUNDATION), Mukrim Abdalla Jaffar, kwajili ya kuwapatia watoto yatima wanaoishi kituo cha Mazizini, Zanzibar.
Naibu Wizara wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanazibar Shadia Mohamed (kushoto), akitoa shukurani zake baada ya kupokea msaada wa vyakula vyenye thamani ya shilingi 5, 462, 000 uliotolewa na taasisi ya (RYTHM FOUNDATION) hafla iliyofanyika ofisi za kituo cha kulelea watoto yatima Mazizini, Zanzibar.
Msaada wa vyakula vyenye thamani ya shilingi 5, 462, 000 vilivyokabidhiwa kwa watoto yatima wanaoishi kituo cha Mazizini, Zanzibar na Taasisi ya Rythm Foundation.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments