Askari wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kama wanavyoonekana. |
Maofisa wa Jeshi wa Jeshi la Magereza |
Wafungwa wakishiriki burudani mbalimbali gerezani ikiwemo onesho la wasanii wana muziki ambao ni wafungwa ikiwa ni sehemu moja wapo ya programu za Urekebishaji magerezani. |
Wafungwa wakishiriki ujenzi wa nyumba za watumishi wa Jeshi la Magereza ikiwa ni sehemu ya kujinza ujuzi wa fani ya ujenzi kama sehemu ya programu ya urekebishaji wahalifu. |
Na ASP. Lucas Mboje, Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza, Dodoma;
Jukumu mojawapo la Maafisa na Askari wa Magereza au Maofisa katika Taasisi za Urekebishaji( *Correctional Services*) popote Duniani ni kazi kubwa katika kuimarisha usalama wa raia na jamii nzima katika nchi husika.
Kama watumishi wa Taasisi/Vyombo vingine vya kiusalama duniani, wanalo jukumu la msingi la kutekeleza programu za urekebishaji wa wahalifu na kutoa ushauri wa kisera kwa Serikali juu ya uzuiaji uhalifu.
Jukumu hili ni zito na nyeti kwa kuwa linagusa maisha ya wananchi wengi na taswira ya taifa kwa ujumla.
Hivyo, Maafisa na askari wa Magereza au Maofisa Urekebu(Correctional Officer's) lazima wawajibike ipasavyo katika kusimamia programu mbalimbali za kuwarekebisha wahalifu ikiwemo kuwafunza stadi mbalimbali za kimaisha(Stadi za ufundi uashi, Seremala, uhunzi na nyinginezo) ili wakitoka nje ya kuta za Magereza wasirejee katika uhalifu.
Aidha, matarajio ya Maofisa Magereza/Maofisa Urekebu na jamii kwa ujumla ni kuona kwamba wafungwa wamalizapo vifungo vyao, wanarudi kwenye jamii wakiwa raia wema. Wanakuwa wameacha matendo maovu na kuendesha maisha yao kama raia wenye mwenendo mwema na wanaotii sheria za nchi.
Pia, wafungwa hao wanaomaliza vifungo vyao wafanye shughuli zilizo halali za kuwapatia riziki zao kwa kutumia ujuzi walioupata wakati wakitumikia vifungo vyao au kabla ya hapo.
Kwa hiyo Taasisi za Urekebishaji(Correctional Services) au Magereza duniani kote wanapaswa kuwafundisha wafungwa stadi za maisha katika nyanja mbalimbali ili wakimaliza vifungo vyao wawe na ujuzi utakaowawezesha kuendesha maisha yao kwa kujitegemea.
Jeshi letu la Magereza Tanzania Bara(Tanzania Prisons Service) pia lina wajibu huo na limeendelea kuwapa wafungwa hawa elimu ya stadi za maisha pamoja na ushauri nasaha ambao hakika unawasaidia kujutia makosa yao ili waishi kama raia wema.
Naamini chombo hiki cha Dola(Magereza Tanzania Bara ) kikitimiza jukumu hilo kwa ukamilifu, kitachangia kwa kiasi kikubwa katika azma ya taifa letu ya kudumisha usalama wa raia, amani na utulivu hapa nchini.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments