Vanessa, Mchumba’ke Gari Limewaka | ZamotoHabari.





Mwanadada ambaye mashabiki wake wa Bongo Fleva wanammisi, Vanessa Mdee ‘V-Money’ na mchumba’ke, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’, ndiyo kwanza gari la mapenzi yao linawaka baada ya kurushiana maneno matamumatamu.

Vanessa analalamikiwa kuwa, mapenzi yamemtoa kwenye reli ya muziki tangu mwaka jana baada ya kunasa kwenye penzi la Rotimi ambaye ni staa wa sinema wa Hollywood, Marekani.

Wawili hao wamekuwa wakieleza ni jinsi gani walivyozimikiana na kwamba wako tayari kwa ajili ya kwenda kwenye neksti levo ya penzi lao kwa maana ya kufunga ndoa.



Juzikati Vanessa alitupia picha akiwa na jamaa huyo kisha kueleza kwamba ndiye mpenzi wa maisha yake.“Love of mya life,” aliandika Vanessa.Naye Rotimi alijibu mapigo kwa kuandika; “Moyo wangu.

”Miezi kadhaa iliyopita, dada wa Vanessa, Mariane Mdee ‘Mimi Mars’ alisema kwa sasa Vanessa ana furaha kuliko kipindi kingine chochote baada ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na jamaa huyo.

 

Imeelezwa kuwa, Rotimi amekuwa akimdekeza na kumpetipeti Vanessa kama malkia kiasi cha kumfanya kusahau muziki.Vanessa alitinga moyoni mwa Rotimi mwaka mmoja baada ya kumwagana na aliyekuwa mwandani wake wa kitambo ambaye naye ni staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini