Waziri Harrison Mwakyembe Atoa Ufafanuzi Jinsi Ligi Zitakavyo Rusishwa "Ligi Kuchezwa Kituo Kimoja, Timu Kugharamiwa" | ZamotoHabari.


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Serikali imeruhusu ligi tatu tu kwa sasa kuanza wakati wakiangalia hali ya maambuzi ya virusi vya Corona yalivyo ili kuzuia maambukizi mapya.


Amesema hayo leo Jijini Dodoma ikiwa ni siku moja imepita baada ya Rais Dkt. Magufuli kutangaza kushuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo ambapo amesema wanategemea sana matokeo ya uchunguzi za afya ili kuruhusu ligi zote kuendelea, ambapo ligi zitakazoanza ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Kombe la shirikisho.

"Kufuatia michezo kuruhusiwa na Mhe. Rais John Magufuli, tunaruhusu Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili pamoja na Kombe la  Shirikisho (Azam Federation Cup) kuendelea ili tupate bingwa pamoja na mwakilishi katika Kombe la Shirikisho Afrika", amesema Dkt. Mwakyembe.

"Viwanja vitakavyotumika kwenye michezo inayotarajiwa kufunguliwa Juni Mosi, 2020 ni Uwanja wa Taifa, Uhuru na Chamazi kwa Ligi Kuu, na Uwanja wa CCM Kirumba na Nyamagana vya Jijini Mwanza kwa Ligi daraja la Kwanza na la Pili", ameongeza Dkt. Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakyembe amesema Serikali itashirikiana na Shirikisho la Soka nchini TFF kuratibu michezo ya Ligi Kuu na ile ya kombe la Shirikisho FA kwa kuchezwa kituo kimoja cha Dar es Salaam na timu zote kugharamiwa kwa bajeti ya shilingi milioni 417 ambayo imetengwa.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini