Alichokisema Shilole Kuhusu Kuongezewa Mke wa Pili na Mumewe "Sintokubali la Sivyo Aniache Mimi" | ZamotoHabari.



Msanii na mfanyabiashara Shilole amesema haitaweza kutokea mumewe Uchebe kuamua kuongeza mke wa pili hata kama dini inaruhusu kuongeza mke mwingine, na akimfanyia hivyo labda aachane naye kisha aoe huyo mwingine.



Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Shilole amesema,
"Nina furaha ndani ya ndoa yangu, ninajiamini na sina mambo mengi ndiyo maana najivunia kuwa na mume wangu,  ni ngumu kuongezewa mke wa pili kwa kweli la sivyo aniache mimi aoe mwanamke mwingine hata kama dini inaruhusu ila mimi sitakubali"
.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini