Kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, msanii wa BongoFleva Alikiba ameghairisha tamasha lake la Kigoma "Behewa la Ukarimu" ambalo alipanga kufanya siku ya Julai 31 mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram msanii Alikiba ameeleza kuwa "Habari ndugu zangu Watanzania, kama wengi mlivyosikia Taifa letu limepata msiba wa baba na mlezi Mzee Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, ni msiba ambao nimeupokea kwa masikitiko imenifikia ghafla sana, lakini ni mapenzi ya Mungu naomba Mungu ampumzishe mahali pema"
"Kutokana na msiba huu mzito nimeahirisha show yetu ya Kigoma iliyokuwa ifanyike Julai 31 ili kushiriki msiba huu wa kitaifa mpaka Agosti 14, pia nimehairisha zoezi la upokeaji michango mbalimbali ambalo nilipanga kulifanya kesho, taarifa za siku ya kupokea michango kwa ajili ya kuweka kwenye Behewa la Ukarimu nitatangaza baada ya msiba kumalizika ahsanteni, natoa pole kwa watanzania na wapambanaji wote walioguswa na msiba huu" ameongeza
Kupitia post zake za nyuma alitangaza kurudi nyumbani kwao kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza mkoani Kigoma baada ya kupita miaka 6.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments