Baba Levo Hits New Milestone Thanks to Latest Song 'High na Low ...Msanii wa Baba levo ambaye pia alikuwa diwani wa kata ya Mwanga kaskazini (ACT-Wazalendo) amesema kinachosukuma wasanii wengi kuingia kwenye siasa kwa sasa ni kitendo cha wabunge waliwapigia debe kipindi cha kampeni kushindwa kufanya kazi yoyote.
Akinukuliwa na kituo cha redio cha East Africa, Baba Levo amesema kitendo cha wabunge na viongozi walipigiwa kampeni wasanii kushindwa kutimiza ahadi yao imefanya wasanii wajione wanaweza kutimiza ndoto na kutatua matatizo ya watanzani.
“Wasanii wengi wameamua kuacha sanaa kuingia kwenye siasa kwa sababu viongozi ambao tulikuwa tunawapigia debe washinde Ubunge hawafanyi chochote zaidi ya kunywa bia, mwisho wa siku wewe msanii na mbunge uliompigia debe wote mnaonekana mmewadanganya watu” amesema Baba Levo.
Mpaka sasa wasanii kadhaa wametangaza nia ya kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia vyama mbalimbali.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments