Balozi wa Indonesia nchini Tanzania avutiwa na uwekezaji Njombe | ZamotoHabari.


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Balozi ,Professa dr Ratra Pardede amesema kuwa atashauriana na wawekezaji wa nchini kwake juu kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani Njombe kufuatia mkoa huo kuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo uzalishaji mbao ufugaji na kilimo cha parachichi na chai.

Akiwa mkoani Njombe Balozi professa dr Ratra pardede ametembelea uwekezaji katika kiwanda cha chai cha kabambe factory Pamoja na kiwanda cha kukamua parachichi kilichopo wilayani wangingo’mbe.

“Baada ya kutembelea baadhi ya wawekezaji wa viwanda hapa Mkoani njombe naamini kutakuwa na ushirikiano baina ya wafanyabishara na wawekezaji kutoka nchini Indonesia na Njombe katika kuuziana mazao mbalimbali baina ya nchi hizi mbili”alisema Balozi Ratra pardede mara baada ya kutembelea kiwanda cha usindikaji na uchakataji wa parachichi cha Olivado

Baadhi ya wawekezaji mkoani Njombe wamesema kuwa ujio wa balozi huyo utasaidia ukuaji wa sekta hiyo hasa katika kubadilishana teklojia Pamoja na kupanua Nyanja ya masoko .

“Kwanza tunashukuru kwa ugeni uliofika katika kiwanda chetu cha Olivado tumepata hamasa kubwa sana,ushirikiano ukiwpo mzuri utatusaidia kwenye maswala kwanza ya miundombinu ikiwa ni pamoja na vifaa au mashine zinazotumika katika uzalishaji wa mafuta”alisema Bosco moja wa kiongozi katika kiwanda cha Olivado

Katarina Revocat ni katibu tawala mkoa wa Njombe amezungumzia ziara ya balozi huyo.

“Tutaweza kuiga njia walizotumia wao hadi kufika pale walipofika,kwa hiyo huu ni wito kwa wananjombe kuangali fursa kama hii ya namna ambavyo tunaweza kushirikiana na Indonesia ili tuweze kupata kupanua masoko ya bidhaa zetu”alisema Katarina Revocati.


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Balozi ,Professa dr Ratra Pardede akitembelea na kujionea uwekezaji na uzalishaji wa majani ya chai unaofanywa na kiwanda cha Kabambe Tea Factory kilichopo Lwangu halmashauri ya mji wa Njombe.



Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Balozi ,Professa dr Ratra Pardede akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha kuhifadhi na kuzalisha parachichi cha Tanzanice kilichopo mjini Njombe.


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Balozi ,Professa dr Ratra Pardede akiwa katika kiwanda cha kusindika parachichi cha Olivado kilichopo wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe alipofika kuona fursa za uchumi zilizopo mkoani Njombe.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini