BancABC yashiriki maonyesho ya 44 ya Saba Saba, yajidhatiti kuimarisha huduma za kibenki | ZamotoHabari.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo akiwasikiliza maafisa wa benki hiyo Advera Ruhiye (Kushoto) na Mariam Haji kuona namna wanavyowahudumia wateja wakati wa maonyesho ya 44 ya biashara ‘Saba Saba’ yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Benki hiyo inatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwamo mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs).
Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo akizungumza na mmoja wa wateja waliotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya biashara ya Saba Saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Benki hiyo imejidhatiti katika kuendeleza biashara ndogo ndogo na za kati kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.Kushoto kwake ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo Charles Silayo.
Maafisa wa BancABC,Hope Madiavalle (Kushoto) na Shazman Karim wakitoa maelekezo kwa wateja waliofika kwenye banda la benki hiyo katika Maonesho ya 44 ya biashara maarufu kama SabaSaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Benki hiyo imejidhatiti katika kuhakikisha inatoa huduma zenye ubora ikiwamo kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.


Benki ya ABC (BancABC) imeshiriki maonesho ya 44 ya biashara maarufu kama Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa utoaji wa mikopo nafuu kwa wateja wake.

Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha hazina wa benki hiyo, Barton Mwasamengo alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na mikopo binafsi kwaajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo kama mamalishe, boda boda na wengine wengi, BancAbc ipo kwaajili ya watanzania wote,” alisema Mwasamengo.

Mwasamengo alisema katika kuboresha huduma imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi.

Mwasamengo alisema benki hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kutoa unafuu kwa wateja wake kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa Corona ikiwamo kutoa unafuu wa riba kwa wateja waliokopa.

“Sisi kama benki tumefungua milango kwa wateja wetu wote waliokopa na ambao hawajakopa, tunataka kuwaendeleza wateja hasa kwa kusikiliza changamoto zao na tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kutoa unafuu wa riba,” alisema.

Vilevile, benki hiyo imeahidi kushirikiana na Serikali katika kuendeleza agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi yaani ‘Financial Inclusion’ kwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia mikopo yenye riba nafuu.

Pamoja na huduma nyingine, benki hiyo ina akaunti ambayo inampa mteja uhuru wa kupokea riba kuanzia riba ndogo kabisa ya Sh10,000 pasipokuwapo na makato ya kila mwezi.Hii imewezekana kupitia mtandao wetu wa kibenki unaowahudumia watanzania nchi nzima.

Aliwahimiza watu kutembelea katika banda la BancABC ili kujionea huduma mbalimbali.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini