Benki ya Dunia yaiweka Tanzania katika nchi zenye uchumi wa kati | ZamotoHabari.


Benki ya Dunia leo imeiweka Tanzania rasmi katika orodha ya nchi za uchumi wa Kipato cha Kati, ikiwa ni miaka mitano kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Kupitia Ukurasa wake wa Twitter, Raisa Magufuli Ameandika ujumbe huu;

"Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai, 2020 imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI.Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya.

"Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020.MUNGU IBARIKI TANZANIA"



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini