BRELA YATOA LESENI ZA VIWANDA, BIASHARA SASASABA, WAFANYABIASHARA WAJITOKEZE | ZamotoHabari.

Kaimu Mkuu wa biashara wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Nimzanael Mchome akizungumza waandishi wa habari katika maonesho ya Biashara yanayofanyika viwanja vya Sabasaa jijini Dar es Salaam.
Mteja Paul Agustino akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Viwanja vya maonesho ya Saasaba.
Mteja wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Hadra Juma akizungumza na waandishi wa haari katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) waalika wananchi wenye biashara zao kusajili biashara, hatanza, leseni za Viwanda pamoja na leseni za biashara kwa muda mfupi katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Blog, Kaimu Mkuu wa biashara wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Nimzanael Mchome amesema kuwa Wapo teyari kuwahudumia kwani wapo na wataalamu wao kwaajili ya kuwasaidia wananchi wanao tembelea banda lao.

Ninzanael amesema kuwa kutokana na janga la Corona Wananchi pia wameitika kusajili biashara zao kwani wanapata watu wengi kwenda kusajili biashara zao.

"Tunatoa huduma ya kusajili papo kwa hapo kutokana na matakwa ya mteja kwani kwa sasa tupo online kwahiyo kila kitu kinafanyika kwa wakati na mtu akitoka anakuwa na cheti cha biashara au kulingana na kile alichokuwa anahitaji."

"Tupo hapa katika maonesho ya Sabasaa kwaajili ya kusaidia na kurasimisha biashara za watanzania huduma tunazotoa hapa tunasajili majina ya biashara, tunasajili alama za biashara, tunasajili makampuni, tunasajili hataza, tunasajili leseni za viwanda pamoja na leseni za biashara." Amesema Nimzanael

Licha ya hilo Ninzanael amewasihi wananchi watembelee katika banda la BRELA kwani wapo mpaka Julai 13,2020 kujipatia huduma kwa haraka.

Kwa upande wa wateja wa BRELA wamesema kuwa huduma zao zipo vizuri kwani wamefanikiwa kupata majina ya kampuni zao kwa urahisi na haraka zaidi.

"Nimefurahia huduma zao kwani nimepata cheti cha biashara yangu moja kwa moja na kuondoka nacho, hivyo nawashauri wafanya biashara kuja kusajili biashara zao hapa sabasaba bila usumbufu wowote" Amesema Hadra

Licha ya Hilo amesema kuwa ukitaka kuomba mkopo benki na hata kama kuomba tenda unaweza kuonesha leseni yako ya biashara na ukapata kwa kuambatanisha pamoja.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini