Freeman Mbowe Ashinda Kura za Maoni Hai kwa 99% | ZamotoHabari.



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ametangazwa kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Hai kwa ticket ya chama hicho baada ya kura za maoni kufanyika leo Hai Kilimanjaro.

Kura hizo za maoni zilihusisha Wagombea wanne na Mbowe ambapo Mgombea Daud amepata kura 2, Irene Lema amepata kura 3, Dorice Mushi amepata kura 28, Edgar Thadei amepata kura 33 huku Freeman Mbowe akiibuka na ushindi wa kura 203 sawa na asilimia 99.

Baada ya ushindi Mbowe amesema “Nawashukuru Viongozi kwa namna ambavyo mmesimamia uteuzi wetu kwa misingi na haki, kila mmoja anatamani kuwa wa kwanza lakini kuwa wa mwisho sio kwamba huna uwezo wa uongozi ila ni kwasababu muda wako bado haujafika, naomba wale wote ambao kura hazikutosha watambue kwamba Chama kinawathamini”

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini