Na. Samwel Mtuwa - DSM.
Leo tarehe 7/7/2020 ambayo ni sikukuu ya Sabasaba Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inayoshirika katika maonesho hayo imewavutia wageni wengi kufika katika Banda hilo wakiwa na hamu ya kuona na kushika Madini mbalimbali yanayopatikana Tanzania kama vile Tanzanite , Dhahabu, Zamaradi, Ganeti ya Nyekundu, Tomalini ya Pinki, Ganeti ya Kijani , pamoja na Madini ya Akwamarini yaliyopo ndani ya Banda hilo.
Sambamba na Madini hayo , kivutio kingine ni mti uliogeuka kuwa Mwamba (Petrified Wood), kutokana na vivutio hivi vya kijiolojia wageni wote wanaofika katika Banda hili wanapata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam juu ya maendeleo ya Utafiti wa Madini na Miamba unaofanywa na GST tangu ilipoanzishwa Mwaka 1925.
Maonesho haya yalizinduliwa rasmi tarehe 3/7/2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , mapema baada ya kuzinduliwa GST imepata fursa ya kutembelewa wageni wengine ambao ni; Profesa Justinian Ikingura ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya GST , Mtendaji Mkuu wa GST Daktari Mussa Budeba , pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne Mama Tunu Pinda.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments