Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewapongeza wadau welevu kwa jitihada zao za kuliunga mkono Jeshi la Polisi na kuliwezesha kujenga kituo kikubwa na cha kisasa na kurahisisha upatikanaji na utoaji wa huduma za kipolisi kwa haraka na wakati.
IGP Sirro amesema hayo akiwa Pangani mkoani Tanga, ambapo alifungua kituo Kikuu cha Polisi wilayani humo kilichojengwa kwa ushirikiano wa wananchi na wadau welevu na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 88.
Aidha, IGP Sirro amewaasa vijana wa eneo la Muheza wilayani Muheza mkoani Tanga, kujikita kwenye shughuli za kujiletea maendeleo na kuacha kujihusisha kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.
Naye Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhe Mwanahasha Tumbo. Amesema ujenzi wa kituo hicho Kikuu cha Polisi ni utekelezwaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba ni lazima askari wawe na maeneo mazuri ya kufanyiakazi pamoja na wananchi kupata huduma bora za kipolisi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments