Kipigo cha jana kwa Yanga kumeiondoa rasmi katika nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ambayo sasa itashuhudia Namungo ambayo itafanya hivyo kutokana na Simba kuwa na tiketi ya uwakilishi katika ligi ya mabingwa Afrika.
Kaimu mwenyekiti wa wanachama wa klabu ya simba sc Mwina Kaduguda maarufu kama Simba wa Yuda amewataka watani wao wa jadi yanga kujipanga upya kutokana na timu hiyo kwasasa haishikiki huku akiwakejeri kuwa safari za nje watazisikia kwa jirani.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa watani wajadi wa nusu fainali ambao simba sc wameifurusha yanga kwa mabao 4-1 Kaduguda amesema yanga sc wanatakiwa kubadilika na kujipanga upya mwakani na kuacha kufanya mambo mdomoni huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kufanya vizuri.
Kwa upande wake aliyekuwa kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Seleman Kova ambaye pia ni shabiki wa Simba ameonyesha kuvutiwa na wachezaji Clatous Chama na Luis Miquisone katika mchezo wa jana ambao wachezaji wote walihusika katika ushindi huo.
Simba sc watakutana na Namungo fc katika mchezo wa fainali utakaopigwa mwezi August mwaka huu katika dimba la Nelson Mandela mkoani Rukwa baada ya Namungo kuwafunga Sahare All star kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyopigwa mkwakwani jijini Tanga
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments