The corona shutdown: Uhuru announces new measuresRais Uhuru Kenyatta amemtaka waziri wa wizara ya Elimu Na ufundi stadi nchini humo kuketi na wadau wanahusika na wizara hiyo ndani ya siku mbili na kutoa taarifa juu Ya kufunguliwa kwa shule nchini humo.
Akizungumza leo wakati akihutubia taifa juu ya usambaaji wa virusi vya Corona Rais Kenyatta amesema kuwa makanisa na misikiti yataruhusia kufunguliwa ndani ya kipindi cha wiki tatu baada ya kujiruthisha juu ya njia za kuwakinga waumini wao.
Aidha Rais Kenyatta amesema maeneo ya ibada hayataruhusu watoto wenye umri chini ya miaka 13 na wazee waliozidi miaka 58, Mikutano na mikusanyiko ya kisiasa yataendelea kusitishwa kwa siku 30 zaidi.
Pia shughuli za usafirishaji wa anga ndani ya mipaka ya Kenya itafunguliwa Jumatano (Julai 8, 2020) huku ndege za kimataifa zikitarajiwa kuruhusiwa ifikapo Agosti 1,2020.
Katika hatua nyingine Rais Kenyatta amesema maeneo ya bar na kumbi za starehe yatafunguliwa kwa wateja kuruhusiwa kununua na kuondoka na sio kukusanyika maneno hayo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments